Aliyemzaba kofi rais wa Ufaransa Macron aeleza sababu za kufanya hivyo (+ Video)

Mwanaume anayeshutumiwa kwa kumzaba kofi Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amefikishwa mahakamani Ijumaa. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 28 amekiri mahakamani kwamba kweli alimzaba Macron, akielezea kitendo alichofanya kuwa cha ”hisia ” na ”ambacho hakikupangwa.”

Amesema kuwa tukio hilo lilikuwa ni matokeo ya decline/ kuzorota kwa hali nchini Ufaransa, kulingana na maelezo yake kwa mahakama.

Mwendesha mashitaka amemuombea Damien Tarel kifungo cha miezi 18 jela kwa kufanya “kitendo cha ghasia kwa makusudi”.

Ofisi ya mwendesha mashitaka ilisisitiza kuwa alikuwa mfuasi wa siasa za mrengo wa kulia zaidi na alikuwa karibu sana na vuguvugu la yellow-vest.

Awali Bw Macron alisema kuwa shambulio dhidi yake halipaswi kupuuzwa na linapaswa kuangaliwa kwa mtizamo usio wa upendeleo.

Rais wa Ufaransa alikuwa akitembea nje ya shule iliyopo katika mji wa kaskazini wa Tain-l’Hermitage alipozabwa kofi na mtu aliyekuwa kwenye kundi la watu waliokua wamesimama nyuma ya uzio wa chuma kwenye eneo la shule hiyo.

Mwanaume aliyempiga kofi Macron alisikika akipaza sauti akisema “Montjoie and Saint-Denis! Let Macron fall”, maneno ambayo yalitumiwa katika vita.

Kulingana na Shirika la habari la Ufaransa AFP, mwanaume huyo alifikishwa katika mahakama ya Valence akiwa bado amevaa fulana aliyokuwa ameivaa wakati alipomzaba kofi rais Macron.

Alipoulizwa ni kwanini aliamua kumzaba kofi rais , alijibu kuwa wakati alipokuwa akiwasubiri marafiki zake, alijihisi kufanya jambo ambalo litakumbukwa.

Alisema kuwa wazo lake la awali lilikuwa ni kumpigia kelele au kumrushia mayai viza rais, lakini alisisitiza kuwa hakufikiria kabisa kumzaba kofi rais.

Kukosoa sera za rais, alisema ilikuwa ni sehemu ya upinzani dhidi ya upinzani wa “yellow jacket” dhidi ya Macron uliofanyika wakati wa urais wake

“Nilijfanya bila kujua,” alisema.

Macron alisema nini kuhusu kofi alilozabwa?

Rais wa Ufaransa awali alikanusha kuwa kitendo hicho kilikuwa ni cha mtu mmoja. Alizizitiza kuwa “watu wa ghasia” hawaruhusiwi kukatazwa kile wanachokidai.

Alielezea tukio katika mkutano na wandishi wa habari akisema: “Kuna wasiwasi wa juu na hali ya mzozo wakati huu ambao haukushuhudiwa wakati wa kipindi cha marais wengine . Lakini kiwango cha mzozo kwa jamii ni cha juu zaidi .”

Alisema kuwa hatahukumiwa binafsi, na amesema ameuachia mfumo wa mahakama kushugulikia suala hilo.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CQA8GluBRjO/

Related Articles

Back to top button