Aliyeua watoto 10 Kenya Masten Wanjala, naye auawa na wananchi

Masten Wanjala mtuhumiwa aliyekiri kuwaua zaidi ya watoto kumi na baadaye kutoroka katika kituo cha polisi alipokua anazuiliwa ameuawa na wanakijiji wa Bungoma magharibi mwa Kenya.

Naibu kamishena wa kaunti ya Bungoma Cornelius Nyaribai amethibitisha kifo chake katika ujumbe wa Twittter.

Polisi wanasema Masten Wanjala alifuatwa na wanakijiji hadi nyumba katika mji wa Bungoma na kupigwa hadi kufa.

Mamlaka ilikuwa imeanzisha msako mkali kumtafuta mtu huyo ambaye alikiri kuwaua zaidi ya wavulana kumi katika kipindi cha miaka mitano.

Masten Wanjala alitoweka kutoka kwa seli za polisi katika mji mkuu, Nairobi saa chache kabla ya kuitikia mashtaka ya mauaji ya wavulana 14.

Maafisa watatu wa polisi wa Kenya waliokuwa kazini siku walifishwa mahakamani siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya kumsaidia mtuhumiwa huyo.

Bwana Wanjala alikamatwa mnamo Julai na alikiri kutumia dawa za kulevya na kuwaua wavulana wadogo, na pia kunywa damu zao katika visa vingine.

Related Articles

Back to top button