Aliyewahi kuwa Meneja wa Harmonize, Mr Puaz azindua Chapa yake ya Mavazi na Viatu

Aliyekuwa meneja wa zamani wa msanii Harmonize hivi karibuni amezindua chapa yake baada ya kimya cha muda mrefu toka ameacha kufanya kazi na Harmonize.

Mwaka 2018 Joel Vicent Joseph au kwa jina Maarufu Mr Puaz aliingia makubaliano na lebo ya muziki ya WCB Wasafi kwa lengo la kumsimami msanii Harmonize lakini baadae mwaka huo huo aliamua kuacha kazi hiyo na kuendelea kufanya shughuli zake.

Hivi karibuni kupitia mitandao yake ya kijamii alifuta picha zake za awali zilizoonyesha kazi zake za nyuma na kuanza kupost bidhaa mbali mbali zikiwemo za mavazi na viatu, kitendo kilichowafanya wengi kujiuliza Kulikoni.

Kuangalia bofya HAPA

Alipoulizwa na bongo 5 kwanini kwa sasa anapost bidhaa mbalimbli alisema kwasasa amezindua chapa yake ya Puaz Shop ambayo itakuwa na chapa mbali mbali zenye jina lake na majina mengine kama ilivyo wasanii au watu maarufu walivyo na chapa zenye majina yao.

Amesema licha ya kuwasimamia wasanii lakini pia kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuwa nanchapa yake upande wa mavazi na viatu na ndipo wazo la Puaz Shop lilipotokea na kulifanyia kazi.

” Mimi ni mjasiriamali na kama mjasiriamali naangalia biashara tofauti tofauti zitakazoniingizia kipato ili maisha yaweze kusonga na ndio maana hata msanii kama Diamond Platnumz hategemei tu muziki ila ana biashara nyingine nyingi na ndio maana na mimi nikaja na chapa yangu ya Puaz Shop ambayo itabeba majina mbali mbali ndani yake na vitu vingi vitakavyokwenda kubadilisha mtazamo mzima wa sanaa ya Mitindo Tanzania kama ilivyo chapa nyingine kubwa duniani kama Prada, Gucci, Covaych, Louis Vuitton ,Versace na nyinginezo nyingi” Asema Mr Puaz.

Kuangalia kwa kina bofya HAPA

Ameongeza pia na kusema hawezi kuacha kusimamia wasanii kwani ni moja ya vitu anavyovipenda sana na ana matarajio makubwa hapo baadae ya kufanya kazi na wasanii wa Tanzania ili kuwavusha na kuwafikisha mbali katika sanaa yao.

Kabla ya kumsimamia Harmonize Mr Puaz ameshafanya kazi na wasanii mbali mbali akiwemo Shetta, Nedy Music na wasanii wengine wengi katuka maeneo tofauti tofauti.

Related Articles

Back to top button