Ally Hapi alivyokifanya kilimo kuwa rahisi machoni, Alikiba amuita ‘Role Model!’ (Picha)
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Tabora na Mara Aly Hapi amekuwa kivutio cha vijana wengi mitandaoni baada ya kujikita zaidi kwenye kilimo na kushare kwa watu wake mtandaoni hatua mbalimbali anazozifanya katika kilimo.
Mwanasiasa huyo ambaye mara ya mwisho alikuwa akihudumu Ukuu wa Mkoa wa Mara na kupumzishwa na Rais Samia Julai 28, 2022 , alikaa kimya kwa muda na baadaye kuibukia mtandaoni akionyesha shughuli zake mpya baada ya maisha ya siasa.
Picha za kilimo ambazo anapakia mtandaoni zimewavutia vijana wengi. Alikiba ambaye na yeye ametangaza kuingia kwenye kilimo, aliandika mtandaoni Ali Hapi ni ‘role model’ kwake.
Baada ya ujumbe huo wa Alikiba, Ali Hapi alimjibu “Thank you Ali. Pamoja we can feed our motherland.,”
Hizi ni baadhi ya pongezi kutoka mtandaoni.
@Alikiba
Role Model
Amranbhuzohera
Replying to AllyHapi. Una inspire Vijana wengi sana kwenye hii agriculture japo kuwa tunacho kiona siyo rahisi kama tunavyo dhania. Behinds it kuna sacrifices ya vitu vingi sana:- Finance, Time, Consistencies nk. Hongera sana brother
JamsheedNassor
Kwenye kilimo au sioo! Safii. Inapendeza, kwa kiongozi kijana, kujenga ushawishi kupitia kilimo, na kuwahamasisha wengine!