Habari

Amuua mdogo wake kwa risasi wakijaribu hirizi kama itazuia risasi

Mvulana miaka 12 kutoka Nigeria ameuawa na kaka yake alipokuwa akijaribu hirizi mpya ya “kuzuia risasi”, polisi wanasema.

Wawili hao waliamini kuwa “wamejiimarisha kwa hirizi ya ulinzi”, kwa mujibu wa polisi katika jimbo la Kwara, Abubakar Abubakar kisha akampiga risasi mdogo wake Yusuf, 12, kwa kutumia bunduki ya baba yao, maafisa wanasema.

Mvulana huyo alipigwa risasi na bunduki ya kizamani inayojulikana kama dane gun, polisi wanasema.

Polisi sasa wanamsaka anayedaiwa kuwa muuaji. Licha ya ukosefu wa ushahidi, hirizi hutumiwa na baadhi ya watu nchini Nigeria ambao wanataka ulinzi dhidi ya matukio mabaya.

Kumekuwa na ripoti kadhaa za watu kuuawa baada ya kupima hirizi na dawa za kishirikina za kuzuia risasi. Haijabainika kwa nini ndugu hao wawili walienda kupata ulinzi. Yusuf Abubakar inasemekana alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa risasi huku kak yake mkubwa akitorokea msituni, polisi wanasema.

Baba wa watoto hao anafanya shughuli za uwindaji. Polisi wamewataka wazazi “kufuatilia shughuli za watoto wao na kuepuka kufanya shughuli fulani zisizofaa”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents