HabariMichezo

Apagawa, aichoma visu TV kisa wametolewa World Cup

Shabiki mmoja wa timu ya taifa ya Mexico alijikuta akii toboa toboa kwa visu TV yake baada ya kushuhudia wakitolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Mexico iliifunga Saudi Arabia 2-1 na kumaliza katika group nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli dhidi ya Polandi waliyokuwa wapili wote wakiwa na alama nne baada ya kukamilika kwa michezo mitatu.

Muda mfupi baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia shabiki huyo wa Mexico alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akiipiga ngumi kioo cha TV yake na kanakwamba haitoshi akatafuta kisu kilipo na kuichoma choma choma.

Imeandikwa na Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents