Habari

Apigwa na Raia wenye hasira kali mbele ya Polisi kwa mauaji ya Jirani yake

Mwanaume mwenye umri wa miaka 55 anayeitwa Chad Irish amejikuta akipigwa na kundi la watu wenye hasira kali mbele ya Polisi kwa ngumi kwa kumuua jirani yake New York Marekani.

Chad amemuua jirani yake huyo mwanadada aliyejulikana kwa jina la Yazmeen Williams mwenye umri wa miaka 31 ambaye mwili wake ulikutwa umefungwa kwenye begi la kulalia kando ya barabara.

Ofisi ya mchunguzi wa afya ilisema kuwa Williams alikuwa amepigwa risasi kichwani na kifo chake kiliamuliwa kuwa mauaji.

Yazmeen Williams alikuwa jirani yake na alikuwa mwana harakati wengi wanasema labda muuaji alitumwa na kulipwa au hawakumpenda jirani yake huyo.

Jamii ambayo mwanamke huyo alipatikana imekasirika siku ya Jumatatu jioni umati ulimsonga Chad Irish alipokuwa akitolewa nje ya nyumba yake kwa machela na kuwekwa kizuizini.

Walianza kupiga kelele za muuaji wakamlaani na kurusha ngumi na kuuliza kwanini amuue mwanamke aliyekuwa jirani ambaye kwa kila hali hakuwahi kuwa na tatizo na mtu yeyote.

Majirani zao wameeleza kuwa Williams hakuwa na shida na mtu alikuwa mpole sana lakini pia alikuwa anapendwa na kila mtu wameeleza kusikitishwa na tukio hilo kwani Williams hakuwa na tatizo na mtu.

 

 

 

 

cc:Freedm News

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents