Michezo

Arafat Haji ataoa ujumbe mzito Yanga

YANGA PRINCESS, Najua tumeshinda Derby Mabinti zangu, najua mna furaha kubwa ila bado tuna safari ndefu ila huu ni mwanzo mzuri sana kufika tulipokubaliana, tukumbuke hatuchezi kwa ajili yetu bali Mamillion ya Wananchi ambao wanaihodhi hii chapa, tunacheza kwa ajili ya ndoto za Mabinti wengi na tunacheza kwa ajili ya heshima ya wote waliovuja jasho tangu Uhuru kwa ajili ya hii chapa ya Wananchi.

Kikosi ni kizuri sana, Mabinti wadogo wenye hali na morali tuendelee kusogea hatua kwa hatua, tukiheshimu mchakato na kikubwa zaidi nidhamu katika hatua zote, tucheze kwa ajili ya nembo kifuani kisha watatukumbuka kwa majina yetu nyuma ya jezi, bado hatujafika ila mwelekeo ni mzuri, pongezi kwa Benchi la Ufundi, Wachezaji, Viongozi na Mashabiki wote mliojitokeza uwanjani na mliotazama kwenye TV.

Nidhamu haipitwi na wakati, Mwenyezi Mungu atubariki sana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents