Michezo

Arsenal kusikiliza ofa ya Aubameyang, Umtiti, Coutinho ndani ya tetesi za usajili Ulaya

Arsenal wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya mshambuliaji wao raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 32, siku chache baada ya kuvuliwa unahodha. (ESPN)

Arsenal 'talking' to Aubameyang successor after January plan confirmation

Napoli wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba na beki wa Everton na Ufaransa Lucas Digne, 28, ambaye amedokeza kuwa anataka kuondoka katika Goodison Park mwezi Januari. (Foot Mercato – in French)kiungo wa safu ya ulinzi Mfaransa Samuel Umtiti

Kiungo wa safu ya ulinzi Mfaransa Samuel Umtiti

Barcelona wanahangaika kumuachilia kiungo wa safu ya ulinzi Mfaransa Samuel Umtiti, 27, na mchezaji nyota wa Brazil Philippe Coutinho, 29, kwasababu wachezaji wote wawili hawataki kuachana na mikataba yao minono katika Nou Camp. (TodoFichajes – in Spanish)

Tottenham wanataka kusaini mikataba na mlinzi na mshambuliaji katika mwezi wa Januari, na wanaangalia namna ya kuwaondoa kwende klabu hiyo mlinzi Matt Doherty, 29, na kiungo wa kati wa England Dele Alli, 25. (The Athletic – subscription required)winga wa Porto na Colombia Luis Diaz

Winga wa Porto na Colombia (kushoto) Luis Diaz

Liverpool wanawafuatilia kwa karibu winga wa Porto na Colombia Luis Diaz, 24, kama mchezaji mbadala wa Sadio Mane, 30, ambaye anaelekea kwenye michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika ambapo atailichezea taifa lake la Senegal mwezi ujao. (FourFourTwo)

Mshambuliaji wa Canada Jonathan David, 21, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal na West Ham, ataondoka katika klabu ya Lille ya Ufaransa mwaka ujao, amesema wakala wake. (Radio Canada – in French)

mlinzi wa England Kieran Trippier

Newcastle inakabiliwa na ushindani kutoka Manchester United na Tottenham katika kinnyang’anyiro cha kusaini mkataba na mlinzi wa England Kieran Trippier, 31, kutoka klabu ya Atletico Madrid. (90min)

Tottenham, Newcastle, West Ham na Rangers wanagombania kusaini mkataba na mlinzi wa West Brom na England Sam Johnstone, 28. (Teamtalk)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents