Michezo

Arsenal wanakwama wapi michuano ya Ulaya

Matumaini ya Arsenal kushinda taji lolote la barani Ulaya yaligonga mwamba usiku wa Alhamisi baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya Sporting Lisbon kutoka nnchini Ureno.

Sporting Lisbon ambao wapo nafasi ya nne kwenye ligi ya Ureno ya Primeira walionekana kuwashika pabaya Arsenal karibia mchezo mzima licha ya Arsenal kufanya vizuri kwennye ligi ya kwao wakiongoza kwa tofauti ya alama 5 mbele ya Man City.

Katika dakika 120 ngumu, Arsenal walikubali bao la kusawazisha la umbali wa yadi 46, lakini pia Arsenal walipoteza wachezaji kutokana na majeraha na mwishowe wakatoka mikono mitupu.

Mikel Arteta anaamini kuwa jeraha la Takehiro Tomiyasu linaonekana kuwa baya sana” baada ya nyota huyo wa Arsenal kuondoka Emirates kwa magongo, huku William Saliba pia akitolewa mapema uwanjani kutokana na tatizo la mgongo.

Ikumbukwe kuwa Arsenal hawajawahi kushinda taji lolote la Ulaya na msimu walionekana kuwa bora zaidi na kuwaaminisha wengi huenda wakaondoka na mataji kadhaa lakini mpaka sasa hawajashinda taji lolote na wamebaki kwenye michuano ya ligi kuu pekee kwanni kwenye m,ichuano yote wametolewa.

Kwa hivyo kushindwa huku, kutaumiza kikosi cha Arteta – ambacho kwa sasa kinaongoza Ligi Kuu kwa pointi tano – au itakuwa ‘baraka’ yenye matarajio makubwa zaidi??

Unahisi Arsenal kutolewa kwenye michuano hii itakuwa kama baraka kwao au ndio mkosi na huenda wakaukosa hata ubingwa wa EPL??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents