HabariVideos

Asha Zungu na mwenzake mbaroni kisa biashara ya ngono mtandaoni (Video)

Kamanda Muliro amesema katika Oparesheni hiyo, watuhumiwa wengine wa makosa ya mtandao pia walikamatwa, ambao ni: Marry Samson Sibora @ ASHA ZUNGU miaka 23, Mzanaki, mkazi wa Sinza Mugabe na Zainabu Yahaya Omary @ official Manka , miaka 23, Mrangi, mkazi wa Buguruni Wanatuhumiwa kwa makosa ya usambazaji wa picha za ngono na kuuza mwili kwa njia ya Mtandao ya kijamii ikiwemo facebook, WhatsApp, Tinder na Exotic tz .

Watuhumiwa wote wamehojiwa kwa kina na taratibu za kisheria zinakamilishwa ili wafikishwe Mahakani haraka iwezekanavyo
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kishria, linatoa onyo kali kwa watu wanao jihusisha na uhalifu kwa njia ya mtandao na njia nyingine, kuwa Serikali na vyombo vyake imejipanga kupambana na uhalifu wa aina yoyote, na wahalifu popote walipo watafuatwa, kukamatwa na kupelekwa Mahakamani.

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Watanzania wote kutumia mitandao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na kuwa waangalifu na vitendo vya utapeli, ikiwemo kuchukuwa tahadhari wakati wa kutuma pesa au kufanya biashara katika mitandao ili kuepuka kutapeliwa, pia watu wajiepushe kufanya biashara haramu mitandaoni kama vile za kuuza mili na ngono.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents