Kufuatia Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuwa katika hali mbaya ya maambukizi ya UKIMWI huku Mkoa wa Mbeya ukiwa nafasi ya pili, wadau wamehamasisha vijana kutumia vipimo maalumu vya mashine za ATM maalumu ya kujipima maambikizi mapya ya virusi vya ukimwi (HIV)
Mashine hizo ambazo zimeanza kufungwa kwenye maeneo ya kumbi za starehe hususan katika Mkoa wa Mbeya huku lengo kuu ni kuona vijana wakihamasika kujipima wenyewe kwa hiari ili kujua hali zao.
Mradi huo wa mashine za ATM zinazotoa vipimo vya ukimwi na kinga unatekelezwa na mfuko wa dharura wa Raisi wa marekani PEPFA na kutekelezwa na shirika la HJFMRI katika mikoa ya nyanda za juu kusini.