Aussems kushuka na vyuma Singida Black Stars
Wakati Singida Black Stars ikiendelea kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao Uongozi wa timu hiyo umesema umemuachia jukumu Kocha Mkuu Patrick Aussems kuamua nani aingie au kutoka kuhakikisha anafikia malengo ya nafasi nne za juu.
Timu hiyo ambayo awali imemshusha kikosini Aussems aliyewahi kuinoa Simba kwa mafanikio kwa kuifikisha robo fainali klabu bingwa Afrika na sasa ataiongoza timu hiyo msimu ujao fainali klabu bingwa Afrika na sasa ataiongoza timu hiyo msimu ujao akisaidiana na Ramadhani Nswanzurimo.
Mkuu wa Idara ya Utawala wa klabu hiyo, Muhibu Kanu alisema hadi sasa mipango yao inaenda vyema ambapo jukumu la nani aingie, kutoka au kubaki limeachwa kwa Kocha Mkuu Aussems.
Alisema msimu uliopita walitamani nafasi nne za juu lakini kutokana na kuipata timu ikiwa chini hawakuweza kufanikiwa na badala yake wanashukuru kubaki salama Ligi Kuu.
“Kwa sasa anapitia ripoti ya benchi la ufundi kisha atatupa tathimini na mapendekezo yake hatuingilii kazi yake isipokuwa tunachotaka ni kutufikisha kwenye Malengo ya nafasi nne” alisema Kanu.
Kigogo huyo ambaye pia ni kocha kitaaluma mwenye leseni A ya CAF, alisema uongozi haswa upande wake anaweza kushauriana na Aussems kwa jicho la kiufundi lakini kazi kubwa ni ya kocha huyo raia wa Ubelgiji.
“Kimsingi lazima wapo watakaoondoka, kubaki au kupelekwa kwa mkopo sehemu nyingine ili kupisha sura mpya tunahitaji, kuona Singida Black Stars mpya” alisema Kanu. Singida ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kung’ara.