Michezo
Ayoub Lakred ni majanga tu

Ofisa habari wa Simba Ahmed Ally amethibitisha majeraha ya mlinda mlango wao namba moja Ayoub Lakred aliyoyapata Misri walipokita kambi ya Maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2024-2025.
“Ni kweli Ayoub ameumia paja na atafanyiwa vipimo atakaporejea kujua kama atatibiwa kawaida ama kwa njia ya upasuaji ,madaktari bado hawajasema atakaa nje kwa muda gani lakini itafahamika mara tu vipimo vitakapokamilika” Ahmed Ally.
Kikosi cha Simba kinarejea nchini hii leo kikitokea Misri ilipoweka Kambi ya wiki 3.