Michezo

Azam FC wamsajili tena kepteni wa Singida United

Klbau ya soka ya Azamu FC, imemsajili tena kiungo Mudathir Yahaya ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Singida United.

Mudathir amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu yake hiyo ya zamani.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa Azam kabla ya kupelekwa kwa mkopo Singida, alimaliza mkataba wake na Azam mwezi Machi mwaka huu.

Azam wameonekana kuzidi kuibomoa ngome ya Singida baada ya kumsajili Tafadzwa Kutinyu na kocha Han van Pluijm.

Related Articles

Back to top button