Michezo
Azam Majeraha yaiandama mno
KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Abdul Suleiman ‘Sopu’ atakuwa nje kwa takribani wiki mbili hadi tatu baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu, katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimamoto kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Daktari wa Azam, Mbaruku Mlinga amefunguka kuwa Sopu atakuwa nje kwa wiki mbili, japo kiungo Yahya Zayd anakaribia kurejea uwanjani kufuatia mwezi uliopita kufanyiwa upasuaji wa goto. .
Dk Mbaruku aliongeza kwa upande wa Sospeter Bajana aliyefanyiwa upasuaji wa nyonga Mei 17, mwaka huu Afrika Kusini, anaendelea vizuri na ameanza programu mbalimbali za mazoezi, hivyo muda wowote atajumuika na wenzake.