Habari

Azam Marine yadondosha meli mpya, ni Azam Sealink I

Kampuni ya meli ya Azam Marine inayofanya kazi Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba hivi karibuni imeingiza meli mpya iliyopewa jina Azam Sealink I.

Meli hiyo ya ya kisasa kinatarajia kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,500 na magari 200.

“Tupo hapa kutoa huduma bora kwa watu wetu,” alisema Meneja Mkuu wa Azama Marine Hussein Said.

Chombo hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma hivi karibuni ambacho kitatumia saa tatu kutoka Unguja kuja Dar es Salaam, saa 4 kutoka Unguja kwenda Pemba na pia kutoka Dar es Salaam kwenda Pemba saa 7.

Kutokana na uwezo wa kubeba magari mengi kwa wakati mmoja unahisi kitakuwa ni chanzo cha kuongezeka kwa magari visiwani Zanzibar kwa kasi? Na je meli hiyo itachangia kukua zaidi kwa shughuli za kiuchumi kati ya Dar es Salaam na Zanzibar?

Related Articles

Back to top button