Mitindo

Aziz Ki analelewa kama Mtoto na GSM – Edo Kumwembe

Hisia zangu zinaniambia Aziz aliamua kusaini Yanga muda mrefu uliopita. Na Ukweli ni kwamba alisaini mkataba mpya Yanga kabla hajaenda likizo nyumbani. Sina uhakika sana kama alipata ofa kubwa kuliko aliyowekewa mezani na Yanga. Ninachofahamu ni kwamba Yanga hapa karibuni walitengeneza mazingira ya kujitekenya kisha kucheka wenyewe. .

Walitengeneza mazingira ya kibiashara katika saini ya Aziz Ki. Kumfanya ang’are na jina lake lichomoze zaidi katika harakati hizi za usajili aonekane kama vile ni mchezaji mpya aliyewasili nchini. Wakatengeneza mazingira kwamba Aziz alikuwa hajasaini kwao wakati walijua wazi kwamba Aziz alikuwa amesaini mkataba mpya.

Hata rais wao, Hersi Said aliwapiga chenga ya mwili waandishi wa Afrika Kusini kwa kuwaambia Aziz hajasaini Yanga halafu ndani ya saa 24 akatangazwa amesaini mkataba mpya. .

Nilifahamu ugumu wa Aziz kuondoka nchini. Aziz analelewa kama mtoto na familia ya GSM pamoja na ile ya Hersi. Yeye, mama yake mzazi pamoja na dada yake wamekuwa familia ya Yanga. Klabu ambayo ilipaswa kumuondoa Aziz nchini ingepaswa kufanya kazi ya ziada. Kuna tofauti ya dau la mshahara au malipo ya kusaini mkataba ambalo lingeweza kumuondoa Aziz nchini, lakini lilipaswa kuwa dau kubwa maradufu. Lilikuwa ni suala dogo tu kwa Aziz kusaini Yanga mkataba mpya tofauti na watu wengi walivyokuwa wanafikiria. .

 

Uamuzi wa Aziz kuondoka au kubaki Yanga unabakia zaidi kwa mama yake kuliko wakala wake. Lakini ukiachana na hayo, kuna raha kubwa ya kuwa Aziz Ki katika Jiji la Dar es salaam na nchi ya Tanzania. Unaishi kwa raha mstarehe. Unaishi kama Ronaldo au Messi. Kila unakopita, kila unalofanya. Jambo hili linawasumbua wanasoka wengi waliopata ustaa nchini. Wawe wa kigeni au wazawa. .

Kwa wageni wengine rafiki zangu kina Mukoko Tonombe waliamua kuoa hapa. Nadhani hii ilimsumbua hata rafiki yetu Fiston Mayele wakati alipokwenda Misri. Akili yake alikuwa ameiacha Yanga na Tanzania kwa ujumla akachukua muda kuzungumzia mambo ya Yanga kuliko mambo ya Misri.” alisema Edo Kuwembe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents