HabariUncategorizedVideos

Baada ya kuona video za CCTV Shahidi kesi ya Sabaya aiomba mahaka impe mapumziko ya kuendelea na ushahidi

Shahidi wa kumi katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake Sita, ameiomba mahakama ipange siku nyingine ili aweze kuendelea na ushahidi wake.

Shahidi huyo amesema hayo Jana  Nov 24 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ambapo amesema baada ya kuangalia matukio ya kwenye CCTV Camera yamemfanya asiwe sawa na kuomba mahakama impe mapumziko ya siku kadhaa kabla ya kuendelea na ushahidi wake.

Shahidi huyo ambaye ndiye muathirika katika kesi ya Sabaya anayejulikana kwa jina la Evarist Mroso amesema siku ya Januari 22 alitoa kiasi cha Milioni 90 baada ya kuambiwa asipofanya hivyo atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na kupotezwa.

Mbali na hayo, Shahidi huyo ameweza kuwatambua baadhi ya watu waliokuwa wakionekana kwenye CCTV Camera, ambao ni mshtakiwa namba 2 aliyekua amevalia kaunda suti ya bluu, mshtakiwa namba sita kama mtu aliyekuwa anamfata kwa karibu sana wakati akiwa anatoa fedha na mshtakiwa namba nne ambaye anatajwa kama baunsa wa Sabaya.

Hakimu anayesimamia kesi hiyo Dk. Patricia Kisinda amekubali ombi la shahidi ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka Nov 29 ambapo shahidi hiyo ataendelea na ushahidi wake.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents