Baada ya Manara kuoa, Diamond asema naye yupo njani kuoa

Baada ya msemaji wa klabu ya @yangasc @hajismanara kutangaza kupitia Instagram yake kuwa ameongeza mke mwingine.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva @diamondplatnumz amecomment na kusema kuwa na yeye yupo njiani kuoa Insh Allah.
Usiku wa jana @hajismanara amefanikiwa kuongeza jiko (kuoa) mke wa pili baada ya miezi kadhaa nyuma kufunga ndoa na mwanamke alienaye kwa sasa.
Hii ni ndio ya tatu ya @hajismanara baada ya mwaka mmoja nyuma kufunga ndoa ya kwanza na miezi mitano iliyopita alifunga ndoa na mwanamke mwingine.
Kupitia mahojiano aliyofanya na media kadhaa @hajismanara alithibitisha kuwa aliachana na mke wake wa kwanza hivyo alibaki na mke mmoja ambaye alifunga naye ndoa miezi kadhaa nyuma.
Hii ni ndoa nyingine ikimaanisha kuwa @hajismanara sasa ana wake wawili baada ya kutangaza kuachana na mke wa kwanza.