Baba akamatwa kwa kuyaondoa matiti ya binti yake mwenye umri wa miaka minane kwa kutumia jiwe la moto

Polisi katika jimbo la Nigeria la Lagos wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwenye umri wa miaka minane kwa kutumia jiwe la moto.

Rekodi ya polisi inasema kuwa baba huyo alitekeleza maasi dhidi ya binti yake, kwasababu matiti yake yalikuwa yameanza kuonyesha ‘chuchu’, ambazo ni ishara za kwanza za kubalehe.

Kwa sasa msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu, huku ripoti zikisema kuwa yuko katika hali mahututi, kutokana na majeraha aliyosababishiwa na baba yake mzazi Bw Banjo.

Baba yake msichana huyo aliripotiwa polisi na kikundi cha kutetea haki za watoto, na Msemaji wa polisi wa jimbo la Lagos DSP Asijebotu amethibitisha madai hayo, akisema kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Kulingana na taarifa nchini Nigeria, wazazi wa msichana huyo kwa sasa wanashikiliwa na polisi katika jimbo la Lagos.

Mkuu wa kikundi cha kutetea haki za watoto Comrade Ebenezer Omejalile, ambacho kilimshitaki baba huyo, ameiambia BBC kwamba Bw Banjo , anayefahamika kama Panel, “Aliyabana na kisha kuyachoma matiti ya binti yake .”

“Baba wa msichana huyo alitumia jiwe la moto alilolifunga ndani ya nguo na kumchoma hadi alipohakikisha kuwa ameyaharibu kabisa matiti ya binti yake,” alisema.

Alisema pia kwamba baba huyo alielezea kutoridhishwa kwake na jinsi binti yake alivyokuwa ameanza kuonyesha dalili za saratani ya matiti kwenye matiti yake, na ndio maana alitaka kuyazuia yasiote.

Mama yake msichana huyo alisema kuwa Bw Banjo amekuwa akimpiga binti yake mara kwa mara.

Comrade Ebenezer alisema kuwa alimwambia baba yake msichana huyo kuwa alifanya uhalifu.

La kusahangaza zaidi ni kwamba, kulingana na Comrade Ebenerzer, ni jinsi baba huyo alivyosema amekuwa kimuogesha binti yake wa miaka 8 kila siku.

Related Articles

Back to top button