Baba Diamond atoa kauli: Naomba aache kutumia jina langu na akaonyeshwe kaburi la baba yake (+ Video)

Baada ya Mama Dangote kuthibitisha kuwa Diamond ana undugu na Ricardo Momo na Mzee Abdul ambaye watu wengi walikuwa wakifahamu kama Baba yake mzazi Mzee Abduli atoa kauli hii.

Bongo5 tumepiga stori na Baba Diamond Mzee Abdul na kusema kuwa yote anamuachia Mungu na kama kweli Diamond sio mtoto wake anamuomba akabadili jina la Mzee Abdul na atumie la huyo baba yake.

Ameongeza kuwa yeye alikuwa hafamu kama Diamond sio mtoto wake na kama kweli Mama Dangote kaongea basi yeye hana jinsi atakubaliana na matokeo ila asitumie tena jina lake akiandika eti ni mzazi wake yaani Abdul.

Related Articles

Back to top button
Close