Burudani
Baba Levo avutiwa na hali ya siasa, aeleza jinsi alivyogaragazwa 2020
Msanii wa muziki @officialbabalevo ambaye pia alikuwa Diwani wa Mwanga Kigoma mwaka 2015 amefunguka kuhusu mswada mpya wa sheria ya uchaguzi ambao umesomwa bungeni wiki iliyopita ambapo amedai hatua hiyo ni nzuri katika ulingo wa siasa.
Akizungumzia suala la kupita bila kupingwa, Baba LEVO amedai kipengele hicho kiondolewe kwani kinatengeneza viongozi ambao hawawezi kuwajibika kwa wananchi.