BurudaniHabari

Baba levo na Harmonize wana ugomvi?? asamehewe na Diamond amefanya kosa gani??

Kupitia kwenye kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameigusia kauli ya Baba levo aliyoitoa Sogea kuwa ataongea na Diamond ili amsamehe Harmonize ingawa hakutaja Kosa.

@el_mando_tz anasema huenda Baba levo alitoa kauli ile kwa sababu Harmonize aliondoka WCB miaka kadhaa iliyopita.

Anasema kuwa kama tatizo ni hilo basi Baba levo amekosea na pia amemkosea Harmonize maana aliondoka WCB n alilipa hivyo hakuna kosa alilolifanya maana laifuata masharti ya mkataba wake kuwa alipe kiasi fulani ambacho kilitajwa kuwa ni milioni 600 then aondoke na alitimiza.

Sio mara ya kwanza Baba levo kuongea kauli hii kuwa ataongea na boss wake ili amsamehe Harmonize, kauli hii itaifanya jamii iamini kuwa Harmonize alikuwa na makosa kumbe hakuna.

@el_mando_tz anasema kama atamuombea kwa Boss wake amsamehe Harmonize, Je unahisi Baba levo atamuombea kwa Diamond amsamehe kwa kosa gani??

Kama ni hivyo unahisi Harmonize ana kosa mpaka aombewe na Baba levo kwa Diamond ili asamehewe??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents