Burudani

“Babu Tale katunukiwa Udaktari, Udaktari upi?” Steve Nyerere (Video)

 

Msanii wa filamu na Mwenyekiti wa Uzalendo kwanza @Steve Nyerere amehoji kuhusu Udaktari wa heshima alioupata mdau wa muziki, Meneja wa Diamond na Mbunge wa Morogoro Kusini Mh. Hamis Tale Tale maarufu kama Babu Tale.

Muigizaji huyo amedai haoni makubwa yaliyofanywa na mdau huyo wa muziki mpaka kufikia kupewa heshima hiyo.

“Babu Tale katunikiwa Udaktari, Udaktari upi?,” aliuliza Steve Nyerere huku anacheka.

Aliongeza “Ni ule aliyetunukiwa Babu Tale basi watu wazima huchutama kwa kusema Babu Tale hongera. Lakini kuna watu wamesoma miaka 19 mambo bado,”

Steve amedai kama ni hivyo basi hata yeye kwa sasa anastahili kuwa daktari mbobezi kwa mambo aliyoyafanya kwa jamii kupitia Taifa hili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents