Bado naendelea na muziki kama kawaida, ukimya wangu ni sehemu ya safari – Marlaw

Muimbaji Marima Lawrence a.k.a Marlaw ambaye hivi karibuni familia yake imeongezeka baada ya mkewe kujifungua mtoto wa pili wa kiume, amesema kuwa bado hajaacha muziki licha ya ukimya wa muda mrefu.

marlawnabesta

Marlaw ambaye ni mume wa msanii Besta na baba wa watoto wawili, ameiambia Bongo5 kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia ukimya wake ni pamoja na majukumu ya familia.

Marlaw na Besta

“Ni kweli nimeingia kwenye familia na familia ina nafasi na ni kitu kikubwa, sijaingia kwa utani, na kama mtu anataka kujua familia ni nini namkaribisha pia aingie aone ikoje, mi nimeingia kiuhalisia kabisa na hiyo ni kitu kikubwa sana kwangu hata kwenye maisha yangu.” alisema Marlaw.

Kuhusiana na ukimya wake hit maker wa ‘Pipi’ amesema yeye bado anafanya muziki na kuahidi kuwa muda ukifika atauvunja ukimya huo.

“Lakini kuhusiana na muziki, muziki upo, na muziki unaendelea kama kawaida, mimi ni mwanamuziki tu kama ilivyo na ni kitu nimechagua na nafanya kwahiyo sidhani kama naweza nikatambulika kwa namna ingine zaidi ya hiyo. Kwa hiyo kama kumekuwa na gap lakini ni kitu cha kawaida sio mbaya litazibwa, kwasababu maisha yanaendelea na shughuli zinaendelea na maandalizi ya kazi yanaendelea, bado kuna mambo mengi yatafata, safari iko njiani bado.” alimaliza.

Related Articles

Back to top button