HabariVideos

Bajeti yawakaba vigogo serikalini

“Viongozi kupimiwa mafuta, baada ya kununuliwa magari wakopeshwe”

Bajeti yawakaba vigogo serikalini“Viongozi kupimiwa mafuta, baada ya kukuliwa magari wakopeshwe”

“Hatua za muda mfupi zitakazochukuliwa ni kupunguza safari za ndani na nje, tutapimiana mafuta ya magari ya serikali kila mwezi, utaratibu huu utatumika hadi kwa wabunge na kupunguza ukubwa wa uwakilishi kwenye mikutano ya ndani na nje.

“Tumezidi mno kupenda ubosi, magari makubwa kwa kila mtu serikalini, matumizi ya starehe katika nchi hiyo hiyo kuna watu wanapata shida kupata mlo mmoja, Rais ameielekeza Wizara ifanye kazi kwenye jambo hili”

“Tutaondoa utaratibu uliozoeleka, dereva na gari anapitishwa chini, bosi anapanda ndege labda kutoka Mwanza au Mbeya anasema tukutane Dar es Salaam na kurudi hivyo hivyo,”

“Kuna utafiti ulifanywa siku moja magari ya serikali 132 yalitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam na yaliyokuwa yanatoka Dar es Salaam yalikuwa 76 kwenye route hiyo hiyo na njiani humo 8 yalikuwa yamepinduka,”-
@mwigulunchemba1

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents