HabariMichezo

Baleke afungua akaunti ya magoli NBC

Imemchukua takribani dakika 45 kwa Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Jean Baleke kufungua akaunti ya magoli kwenye Ligi Kuu ya NBC na timu yake.

Baleke amefunga goli pekee na kupeleka furaha kwa mashahiki wa Simba baada ya mpira kumapizika kwa Dodoma Jiji kupoteza mchezo huo.

Simba hii leo wameshuka uwanjani huku wakiwakosa baadhi ya wachezaji wao kutokana na majeruhi na wengine kuwa na kadi tatu za njano.

Baadhi ya mastaa waliokosekana Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji.

Wachezaji wenye kadi tatu za njano ni pamoja na Pape Sakho, Joash Onyango, Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute.

Wachezaji wanaotajwa kuwa na majeruhi ni pamoja na Moses Phiri, Peter Banda, Henock Inonga, Clatous Chama na Jonas Mkude

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button