HabariMichezo

Baleke atawafunga Yanga goli tatu- Ahmed Ally

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ametupa dongo kwa watani zao Yanga akidai kuwa mchezaji wao hatari kwa sasa Jean Baleke ataondoka na mpira siku akimaanisha kufunga goli tatu ‘hat-trick’ watakapokutana Aprili 16.

”Jana hatujalala tumekesha tunabembeleza Baleke alikua analia usiku kucha analalamika kwanini hajaondoka na mpira kwenye mechi ya Ihefu. Ikabidi tumuahidi kuwa ataondoka na mpira April 16 ndo akanyamaza.”- Ahmed Ally

Maneno hayo ya Mzee wa ‘Kispika’ nikama ana ‘Wafokea’ Wananchi wajipange kisawasawa kutokana na uwepo wa mfungaji huyo raia wa Kongo Jean Baleke.

Baleke mpaka sasa amefikisha jumla ya magoli saba (7) Ligi Kuu ndani ya kipindi kifupi tangu asajiliwe na Simba kwenye dirisha dogo.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents