Michezo

Bao pekee la Ronaldo laipatia ushindi Ureno dhidi ya Morocco kombe la dunia

Nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuipatia ushindi timu yake ya taifa ya Ureno dhidi ya Morocco baada ya kutupia bao pekee na la ushindi kwenye mchezo huo wa michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi.

Ronaldo amefunga bao hilo kunako dakika ya nne kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo huo uliyopigwa kwenye dimba la Luzhniki kumalizika kwa matokeo ya Ureno 1 – 0 Morocco.

Kwa bao hilo linamfanya,  Ronaldo kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kimataifa kuliko mchezaji yeyote yule barani Ulaya katika historia ya mchezo wa soka na matokeo ya leo yanaiweka Ureno kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hii baada ya kujikusanyia alama nne kwenye michezo yake miwili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents