Michezo

Barcelona yaanika Ufalme wa Messi, yatoa sababu hizi 17 kwanini yeye ni bora kuliko Kiumbe mwingine katika soka 

Miamba ya soka nchini Hispania klabu ya Barcelona kupitia website ya timu hiyo imetoa sababu 17 ambazo zinamfanya nyota wake, Lionel Messi kuwa mchezaji bora zaidi duniani kuliko mwengine.

Image result for mess best player

1. Taji la La Liga na Spanish Super Cup

Baada ya ushindi wa mataji mawili msimu uliyopita, Lionel Messi imemfanya kuwa na jumla ya 34 kwa mataji yote aliyowahi kuchukua hivyo kuwa ‘top’ katika historia ya Barça.

2. Mfungaji bora wa La Liga

Messi amefunga jumla ya mabao 36 katika mechi 34 alizocheza kwenye ligi msimu uliyopita na kuiyongoza Barça kufikisha jumla ya makombe 26 ya La Liga championship, na mataji sita ya Pichichi Trophy kama mfungaji bora wa ligi.

3. Mshindi wa European Golden Shoe

Ukiachia mbali kutwaa taji la Pichichi Trophy lakini pia Messi ameshinda kiatu cha dhahabu ‘Golden Shoe’ kama kinara wa utupiaji mabao.

4. Mfungaji bora wa UEFA Champions League

Messi aliweza kuiyongoza klabu yake kwenye michuano hiyo kwa kufunga mabao 12 katika michezo 10 aliyocheza.

5. Mabao 600 ndani ya klabu yake ya Barça

Mbali na kuweka rekodi isiyogusika lakini pia, Messi ndiye anayeongoza kwa kupachika mabao ndani ya klabu yake ya Barcelona na kuwa mfungaji bora wa muda wote.

6. Anaongoza kwa magoli ya ‘free-kick’ ndani ya European leagues

Leo Messi amefunga magoli sita (6) kwa njia ya free-kick msimu wa mwaka 2018/19, hivyo humfanya kuwa mchezaji pekee aliyepicha mabao hayo kuliko mwingine yoyote kwenye ligi za Hispania, Ufaransa, Italia, Ujeruman na Uingereza. Kama utajumlisha na yale mawili aliyofunga kwa njia kama hiyo ya ‘direct-free-kick’ kwenye michuano ya Champions League inakuwa jumla nane.

7. Mabao 400 ndani ya La Liga

Hapo haijatosha, Messi anakuwa mchezaji wa kwanza kufikisha jumla magoli 400 kwenye ligi kuu ya Hispania rekodi ambayo haijafikiwa na mtu mwengine.

8. Akifunga zaidi ya mabao 50 kwa misimu sita mfululizo

Idadi hii ikijumlisha mashindano yote, Messi amefunga mabao hayo 51 kwenye michezo 50 na kumuweka kwenye ramani nyingine ya soka. Mabao hayo 36 kwenye La Liga; 12 katika michuano ya Champions League na yale 3 akifunga kwenye Copa del Rey.

mini_3200x2000-MESSI_51_GOLS-

9. Rekodi ya kushinda mechi nyingi zaidi katika historia ya La Liga

Messi ameweka rekodi hiyo ya kushinda mechi nyingi zaidi za La Liga kkuliko mchezaji mwingine na kumpiku aliyekuwa golikipa wa Real Madrid, Iker Casillas kwa kushinda mara 334 .

10. Rekodi ya kushinda mara nyingi zaidi katika historia ya Barça

Messi alimpita Xavi na kufikisha 477 mechi alizoshinda akiwa na Barcelona kwa michuano yote, wakati mkongwe Xavi akistaafu na kumuacha mchezaji huyo bora wa dunia kwa mujibu na FIFA akiendelea soka.

11. Rekodi ya kuisaidia Barça kutwaa makombe mengi zaidi ya La Liga

Messi ni mchezaji pekee anayeongoza kuisaidi klabu ya Barcelona kutwaa mataji mengi ya La Liga, na hii ni kutokana na muda aliyokaa na nafasi nyingi alizopata kucheza ukilinganisha wengine ndani ya timu hiyo.

mini_FCB_Liga-Victory_Header

12. Mfalme wa assists ndani ya La Liga

Ukiachiambali kuwa kinara wa kutupia mabao, lakini Messi ameongoza kwa kutoa pasi nyingi za mwisho ‘assits’ zilizochangia kupatikana magoli, akitoa (assists) 13.

13. Copa América bronze medal

Messi ameiyongoza timu yake ya taifa ya Argentina kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Copa América, ambapo walikuja kukwama dhidi ya Brazil, kabla ya kushinda mshindi wa tatu mbele ya Chile.

14. Rekodi ya kufunga zaidi ya magoli 20 katika La Liga kwa misimu 11 mfululizo

Messi ni mchezaji pekee kufunga zaidi ya idadi ya magoli 20 kwa kila msimu huku akifanya hivyo kwa misimu 11 mfululizo mpaka sasa hii ikiwa ni tangu mwaka 2008/09.

15. Zaidi ya magoli 50 akifunga kwenye Copa del Rey tangu kuanza kuitumikia Barcelona

Mabao matatu ya Copa del Rey aliyofunga msimu uliyopita yanamfanya Messi kufikisha idadi ya jumla ya magoli 51 katika kipindi chake chote na kuwa nafasi ya pili baada ya kwanza kuchukuliwa na Josep Samitier (1919-1932), akitupia magoli 64.

16. Akifunga hat-trick 50

Mabao matatu aliyofunga dhidi ya Sevilla msimu uliyopita yanamfanya mwanaume huyo kufikisha (hat-trick ) ya 50. Wakati (hat-trick ) 44 akiifungia klabu yake ya Barça na sita (6) akiwa na Argentina.

17. Rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali sita tofauti za Copa del Rey

Bao la Messi dhidi ya Valencia limemfanya kufikia idadi hiyo, licha ya goli hilo Barcelona haikuweza kutwaa kombe hilo.

Takwimu zote hizi ni kwa mujibu wa Website ya klabu ya Barcelona ikiandikwa na Hamza Fumo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents