Burudani

Barnaba wajibu wanaouliza kwanini amebadili dini kisa mwanamke kupitia wimbo “Nampenda” (Video)

 

Kwa sasa @barnabaclassic anaitwa Mohamed baada ya kubadili dini na kuwa muislamu kumfuta mke wake mtarajiwa Raya ambaye amekuwa kwenye mahusiano kwa miaka mingi.

Baada ya maneno mengi kuhusu tukio hilo, muimbaji huyo ameachia wimbo “Nakupenda” ambao unaeleza mambo mengi kuhusu mahusiano yake.

Barnaba amedai watu hawajui alipotoka na Raya kwani walishaachana mara kadhaa na kurudiana na mapenzi yao yanakuwa mapya kabisa.

Mashabiki kupitia mtandao wa YouTube wameonekana kuupokea kwa mikono miwili wimbo huo huku wengi wakisifia uandishi wake.

Kwa sasa video ya wimbo huo inapatikana YouTubu kupitia link iliyopo kwenye bio ya @barnabaclassic .

Written and edited by @yasiningitu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents