Habari

Barrick Bulyanhulu yaendelea kurudisha kwa jamii kwa kutekeleza miradi mbalimbali

Katika kuhakikisha wananchi wananufaika na uchimbaji madini, Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika wilaya za Kahama na Nyang’hwale mkoani Shinyanga umeendelea kuisaidia jamii zinazozunguka mgodi huo kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali na barabara.

Hayo yamebainishwa na Meneja Masuala Endelevu wa mgodi huo, Agapiti Paul wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji uliyofunguliwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Paul amesema wameendelea kuzijali jamii zinazozunguka mgodi kwa kuhakikisha zinanufaika na uwepo wa madini katika maeneo yao kwa kuwajengea barabara, hospitali pamoja na shule ambayo imechangia kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi.

“Hata hivyo tunajali masuala mazingira kwa ujumla kwa kuyarudisha katika hali ya awali maeneo yote ambayo wanayachimba na kutolewa madini, tunafanya kazi mbalimbali kwa kuhakikisha jamii inaozunguka mgodi inanufaika. mfano katika mgodi huu wa Bulyanhulu tumefanya miradi mingi ikiwemo ujenzi wa hopsitali, barabara, shule ambayo imechangia ongezeko la ufaulu wa wanafunzi,” amesema Paul

Aidha Paul amesema kuwa katika migodi yao wamekuwa wakihakikisha wanachimba madini kwa njia ambayo ni salama na kujali wafanyakazi wao pamoja na jamii zinazowazunguka.

“Tutaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunakuza uchumi na pato la taifa kupitia madini, tuwahamasishe watanzania wengine kukuza uchumi hususani kupitia sekta hii ya uchimbaji madini, Barrick tunajivunia kuwa sehemu ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania,” amesema

Hata hivyo Paul amesema mkutano wa kimataifa wa madini na uwekezaji ni muhimu kwa watanzania hasa kwao kwani ni moja ya mahali ambapo wanaonesha ni kwa jinsi gani wanafanya uchimbaji wa madini kwa njia ambayo endelevu.

“Katika migodi yetu tunahakikisha kwamba yale madini ambayo tunayachimba basi yanachimbwa kwa njia ambayo ni salama, lakini pia tumekuwa tukiwajali wafanyakazi wetu pamoja na jamii inayotuzunguka,” amesema

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents