Burudani

BASATA watangaza mabadiliko ya bei za usajili, MaDJ na Wasanii wapumua, Makampuni bei juu

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) leo July o4, 2018 limetangaza mabadiliko ya gharama za usajili zilizotangazwa mwezi Februari mwaka huu.

Related image

Kwenye mabadiliko hayo wasanii wanaotoka nje ya nchi watapata kibali cha kufanya kazi nchini kwa ada ya shilingi milioni 1.5  hii ni kwa wasanii ambao wanatoka nje ya Afrika Mashariki.

Wasanii wanaotoka nchi za Afrika Mashariki watatozwa ada ya kibali shilingi milioni 1 na kwa dharura yoyote ile msanii kutoka nje atatozwa tsh milioni 2 .

Katika mabadiliko hayo, gharama za usajili wa MaDJ, Wasanii, Mapromota na Lebo za muziki zimepungua huku gharama za kujisajili kwa msanii mmoja mmoja zikibaki vile vile shilingi elfu 20 .

Kwa upande mwingine, Makampuni yatakayotumia wasanii au sanaa kujitangaza (Branding) yatatozwa gharama ya shilingi laki 5 huku matangazo yatakayotumia wasanii kila tangazo/tukio litatozwa shilingi milioni 5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents