Batuli kufuata nyayo za Kanumba, ajipanga kuandaa filamu yenye bajeti kubwa

Msanii wa filamu nchini, Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli amesema mashabiki wake wa filamu wasione yupo kimya kwakuwa yupo kwenye mpango kuthubutu kama alivyothubutu marehemu Steven Kanumba kwa kuaanda filamu itakayogharimu zaidi ya shilingi milioni 40.

10932487_1474070292904885_331977477_n

Batuli ameiambia Bongo5 kuwa licha ya kuwa anafanya filamu zilizozoeleka, anajipanga kufanya kitu kikubwa ili kuipa heshima tasnia ya filamu nchini Tanzania.

“Kazi zangu zinaenda bomba lakini kuna kazi ambazo zinahitaji udhamin Kwa sababu ni kazi tofauti na hizi zilizozoeleka.Inahitaji watu wengi, kazi inayohitaji milioni 40 na kuendelea. Kwahiyo tunahitaji udhamini kwa sababu ni tofauti na filamu hizo ambazo tumezizoea,” amesema muigizaji huyo.

“Ni filamu ambayo ipo kijamii zaidi, imezama ndani zaidi, yaAni nafanya kitu kikubwa bila kujua nitapata nini. Nataka kuthubutu kama alivyothubutu Kanumba na ndo maana nipo cool nahangaikia udhamini ili nikamilishe hili. Mpaka sasa hivi huu ni mwezi wa 5 nipo kwenye maandalizi na bado naona itafika mpaka mwezi wa 12, kwahiyo wadau wasubirie. Ila pia kuna kazi filamu hizi za kawaida zitaendelea kutoka,” ameongeza Batuli.

Katika hatua ngingine Batuli amewapongeza wasanii waliojitokeza kugombea nyadhifa mbalimbali za siasa huku yeye akitoa sababu ya kukaa pembeni kwa wakati huu.

“Mimi nitatangaza nia yangu wakati ukishafika, inawezekana labda kuna kitu nakitaka labda sio uwaziri labda ni kitu fulani ambacho kinafanana na kitu kama hicho. Pia nawapongeza wote waliotangaza nia, wameonyesha kujiamini. Pia naomba wawapokee wasanii wenzangu sio wote ila wale ambao wanawaona wanafaa kwa sababu sio wote wanafaa hata kwenye watu kumi kuna wa kwanza mpaka wa kumi. Kwahiyo wawapokee wasanii wenzangu kwenye siasa.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW