HabariMichezo

Bayern Munich kumrejesha Ronaldo Ulaya ?

Mfanyabiashara, Markus Schon amesema kuwa wapo tayari kutoa dili nono litakalomrudisha mchezaji ghali zaidi duniani, Cristiano Ronaldo barani Ulaya na kujiunga na vigogo wa Bundesliga Klabu ya Bayern Munich.

Markus Schon amedai kuwa huwenda, Ronaldo akatua Ulaya msimu huu majira ya joto kujiunga na Bayern.

Kwa sasa Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji soka anayelipwa mkwanja mrefu zaidi akiwa na timu ya Al-Nassr inayoshiriki Saudi Pro League lakini ripoti za kurejea Ulaya zimezidi kutikisa mitandao ya kijamii.

Wachambuzi wanasema kama Ronaldo mwenye umri wa miaka 38, anatarajia kushiriki tena michuano ya Champions League basi kutua Bayern Munich ni sehemu sahihi zaidi kwake.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents