Habari
BBC wazindua Komla Dumor award, mtanzania atakayeshinda kuishi Uingereza miezi mitatu (+Video)
Shirika la utangazaji la BBC leo Januari 17, limezindua rasmi tuzo za Komla Dumor kwa mwaka huu wa 2023 jijini Dar es Salaam. BBC imewataka waandishi wa habari wa Tanzania kutumia fursa hiyo kutuma maombi ya aina ya wazo la habari ambalo mtu angependa kulifanyia kazi na wao watalipitia kisha watamuwezesha kwa kumchukua kwenda jijini London, Uingereza na kupewa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu pamoja na kupata nafasi kwenye Dira ya Dunia hya BBC.