HabariMuziki

Behani na ujio wa ngoma -LET ME KNOW

Kutoka Delectable Music staa wa muziki mzaliwa wa Austaria ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani Rebekah Behbahani maarufu kama Behani ameachia kazi yake mpya iitwayo LET ME KNOW inayopatikana ulimwenguni kote.

Staa huyo mwenye vipaji lukuki kama vile mwimbaji mzuri, mwandishi wa wimbo, mtunzaji na muandaji wa muziki Ametoa kazi hii kuwapa Furaha mashabiki zake.

Behani amefanya kazi na mastaa Wakubwa kama French Montana, na Scott Storch ambaye anatarajia kuachia kazi yake mpya na Ne-yo siku zijazo.

Kiufupi tu! Behani Rebekah Behbahani alizaliwa huko Melbourne, Australia ni binti wa mzee Kiajemi na mama yake anaasili ya Italia. Enzi za UTOTO wake Behani alionesha niya yake ya dhati ya kupenda muziki na aliwasikiliza sana wasanii kama Nelly Furtado Beyonce na Britney Spears.

Hapo ndipo alijenga sauti yake ya uimbaji na aliweza kuimba katika ukumbi na muziki shuleni na kuandika nyimbo zake mwenyewe. Baadae alipata nafasi Iconic Mega-Producer Scott Storch (Dr Dre, Beyonce) ambaye alimkaribisha studio, na alishirikiana na ne-yo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents