Habari

Bei mpya za mafuta, 3,410 petroli na dizeli 3,322 mafuta ya taa 3,765 Dar Es Salaam

Siku ya leo Bei ya mafuta nchini Tanzania, imepanda tena mwezi huu na kuivuka ile ya Julai 2022 ambapo petroli imepanda kwa Sh190 kwa kila lita na Sh179 kwa kila lita ya dizeli huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh323 kwa kila lita kwa Jiji la Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumanne Agosti 2, 2022 na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), bei ya rejareja jijini Dar es Salaam itakuwa Sh3,410 kwa lita moja ya petroli na Sh3,322 kwa dizeli huku mafuta ya taa yakifika Sh3,765.

Kutokana na bei hiyo mpya ambayo itaanza kutumika kesho, petroli imepanda kwa Sh190 kwa kila lita ambapo mwezi uliopita iliuzwa Sh3,220 na Sh179 kwa kila lita ya dizeli ambayo mwezi uliopita iliuzwa Sh3,143 huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh323 kwa kila lita ambako mwezi uliopita yaliuzwa Sh3,442.#Bongo5Updstes

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents