Michezo

Benchikha Jwaneng ni jeshi lisilotabirika

Kocha wa Wekundu wa Msimbazi Abdelhak Benchikha amesema “Jwaneng Galaxy sio timu rahisi ni kama jeshi lisilotabirika, hakuna aliyedhani kama ingeifunga Wydad Casablanca nchini Morocco kwenye mchezo wa kwanza wa makundi, hata hapa Simba rekodi zinaonuyesha wamewahi kushtua kwa kushinda hapa nadhani mashabiki na hata wao wachezaji wanalijua hili na tayari nimeshakaa kakao na wachezaji na kuwakumbusha.”

“Kwenye soka mambo ya kushtua Kama haya huwa yanatokea, sitaki historia hii ijirudie hapa chini yangu, nimezungumza na wachezaji tukiwa nao kule ugenini juzi nadhani kila itu ataelewa tulizungumza nini. Tunatakiwa kujipanga tu na vita nzito ya mchezo huu, nawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kuwapa hamasa wachezaji wao wakiwa vitani ndio kitu pekee tunahitaji kutoka kwao.”

“Ili kushinda mchezo huu tunahitaji kufunga mabao yakutosha lakini pia kujilinda vizuri kule mbele bado hatujawa imara tutawaongezea wachezaji mbinu za kutengeneza nafasi na kuzitumia kwenye hizi siku tutakazokuwa kambini.”

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents