Michezo
Benjamin Asukile akutana na rungu la TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limenfungia michezo mitano na faini ya shilingi 500,000 mchezaji wa Tanzania Prisosns Benjamin Asukile.
Kamati ya mashindano ya TFF ilipitia ripoti mbalimbali za michezo ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) baada ya kumalizika raundi ya Tano ikiwemo mchezo namba 094 kkati ya Tanzania Prisons na Young Africans.