Habari

Benki ya CRDB yanyakuwa tuzo tatu usiku wa Consumer Choice Awards Africa 2023

Benki ya CRDB yaweka historia kwa kushinda idadi nyingi ya vipengele vilivyokuwa kwenye Comsumer Choice Awards Africa 2023 kwa kupata tuzo tatu.

Hii imetokana na ufanisi mkubwa ambao Benki ya CRDB imekuwa nao kuhakikisha wateja wake wanapata huduma zinazokidhi mahitaji yao ya kifedha.

 

Kwenye tuzo hizo zilizotolewa mbele ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Dotto Biteko, Benki ya CRDB iliondoka na tuzo ya benki yenye mtandao mpana wa ATM zinazotoa huduma, benki kubwa inayotoa huduma bora kwa wateja huku Mkurugenzi wetu Mtendaji, Abdulmajid Nsekela akitambuliwa kama mkurugenzi mwenye ushawishi zaidi Tanzania.

Ushindi huu ni kwa wateja wetu wote asanteni sana kwa kuendelea kutuamini.

#CRDBBank
#ccawardsafrica2023

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents