Benki ya Exim Tanzania Yaleta ‘Elite Banking’ Arusha naKilimanjaro

Baada ya uzinduzi wa huduma yaElite Banking jijini Dar es Salaam, Benki ya Exim sasayasogeza huduma hii kwa wateja wake wa Arusha naKilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kutoa hudumabora na za kipekee kwa wateja wake kote Tanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha waBenki ya Exim Tanzania, Bw. Shani Kinswaga,“Kiini cha uzinduzi huu kilikuwa ni kuanzishwa kwa falsafa mpya ya‘Kufafanua Upya Dhana ya Upekee’. Huduma hii siyo tu yakifedha, bali ni ahadi yetu ya kuwapa wateja hudumazinazoendana na mahitaji na ndoto zao. Kupitia suluhisho bora za kifedha, ushauri wa kitaalamu, pamoja na timu maalum yawasimamizi wa mahusiano, Elite Banking inakuja na kiwangokipya cha huduma ya kisasa na rahisi. Kusogeza huduma hiiArusha na Kilimanjaro ni sehemu ya maono yetu ya kuhakikishawateja wetu wote nchini wanapata huduma za kipekee na za kisasa.”
Aliongezea kuwa Elite Banking inazingatia nguzo kuu tatu: Ubora wa hali ya juu, huduma za kipekee, na Urahisi. Ubora wakipekee unaokuja na viwango vipya katika huduma za kibenkikwa kuwasogezea wateja wetu ulimwengu wa huduma za kidigitali karibu zaidi popote walipo duniani, fursa za maisha nasuluhisho za kifedha. Huduma ya kipekee yenye timu maalumya usimamizi wa mahusiano na mteja anaweza kufurahiamaeneo maalum ya mapumziko. Urahisi na usisamizi wakifedha usio na usumbufu.
“Hii siyo tu huduma ya kawaida ya kibenki, bali ni hudumamaalum na ya kipekee iliyobuniwa kwa ajili ya kutambuamahitaji ya mteja na kusaidia mteja kutimiza ndoto na malengoyake ya kifedha”
Uzinduzi huu unajengwa juu ya msingi imara uliowekwa nahuduma ya ‘Preferred Banking’ iliyoanzishwa mwaka 2016, nasasa unavuka mipaka kwa kutoa suluhisho za kibenki za kipekeekwa haraka na kwa ubora zaidi, Benki ya Exim inajivuniakuwaletea wateja wake huduma hii ya Elite Banking.
Elite Banking inajumuisha faida mbalimbali kama vile sehemu maalum za mapokezi ndani ya matawi, usafiri wa kimataifa kupitia Mastercard, ushauri wa kifedha binafsi, na mipango ya kifedha iliyoundwa kulingana na malengo ya mteja. Kila mtejaanapata Meneja wa Mahusiano anayetoa ushauri kulingana namahitaji ya mteja.
Bw. Andrew Lyimo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Rejarejakatika Benki ya Exim, aliongezea “Elite Banking iliundwa kwalengo la kuwapatia wateja wetu safari ya kibenki inayolinganana malengo yao. Kwa kuunganisha wateja na ubora wa kipekee, huduma zilizorahisishwa,fursa mbali mbali zinazolengakumwezesha mteja kwa ujumla.
Benki ya Exim imeungana na Mastercard kuleta Mastercard World Card Suite inayojumuisha kadi tatu: Mastercard World Debit Card (TZS), Mastercard World Debit Card (USD), na Mastercard World Credit Card. Kila kadi imeundwa kutoaurahisi wa kimataifa, na suluhisho za kifedha zinazokidhimahitaji ya wateja.
Bw. Andrew Lyimo aliongezea kuwa ushirikiano huu naMastercard unakuja na manufaa mengi ikiwemo urahisi wakupata maeneo maalum ya kusubiria kwenye viwanja vya ndegekote duniani (DragonPass) zaidi ya 1,000 duniani, hudumamaalum za kipekee na huduma za usafiri wa kifahari, pamoja nabima kamili ya kusafiri inayojumuisha kila kitu kuanzia ajalihadi matibabu ya dharura. Wamiliki wa kadi hizi pia wanapataulinzi thabiti wa manunuzi duniani kote, pamoja na zawadi za kipekee kwa ajili ya manunuzi, milo, usafiri, na burudani, zotezikiendeshwa na teknolojia ya kisasa ya malipo isiyotumia fedhataslimu.
Kwa kuileta Elite Banking, Benki ya Exim inathibitisha nafasiyake kama mshirika wa kuaminika katika safari za kifedha, ikileta upekee kupitia huduma za kibinafsi, zinazohusiana namahitaji, na zenye manufaa ya kweli.
Zaidi ya urahisi wa matumizi, Wamiliki wa kadi pia hufurahiaulinzi imara wa ununuzi wa kimataifa, Mifumo ya hali ya juu yakuzuia ulaghai, na program za kipekee za zawadi zilizoundwamahsusi kwa ajili ya chakula, manunuzi,usafiri naburudani.Huduma hii ina teknolojia ya kisasa ya malipo bilakugusa, Mastercard World card Suite inahakikisha kila muamalani salama,rahisi na wa kipekee ambayo ni msingi na lengo kuula Elite Banking








