HabariMichezo

Benzema kulikosa Kombe la Dunia Qatar

Mwezi mmoja tu baada ya kujishindia tuzo ya mchezaji bora wa kandanda “Ballon d’Or”, ndoto ya Karim Benzema ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia inayoanza leo huko Qatar imetoweka baada ya kupata jeraha katika paja lake la kushoto wakati wa mazoezi hapo jana.

Timu ya Ufaransa ambao ni mabingwa watetezi, wanakabiliwa na changamoto kubwa baada ya wachezaji wake kadhaa kupata majeraha na hivyo kutoweza kushiriki michuano hiyo muhimu.

Miongoni mwao ni Paul Pogba, N´golo Kante na Christopher Nkunku. Wenyeji Qatar wataingia uwanjani leo jioni kupambana na timu ya Ecuador katika mechi ya ufunguzi kwenye michuano hii ya Kombe la Dunia itakayomalizika Desemba 18.

Related Articles

Back to top button