Michezo

Bibi wa miaka 100 mwenye rekodi ya kukimbia mita 100 kwa dakika moja

Ida Olivia Keeling ni mwana riadha kutoka nnchini Marekani  mwenye umri wa miaka 100 aliyeweka rekodi ya kukimbia mita 100 ndani ya dakika 1 na sekunde 17 akiwa kibibi wa miaka 100.

Akiwa na umri wa miaka 100, Mwanariadha huyo wa New York Ida Keeling ameweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za mita 100 kwa wakimbiaji wenye umri wa zaidi ya miaka 80, akikimbia kwa muda wa dakika 1 na sekunde 17.

Ida Keeling, ambaye pia anashikilia rekodi ya kuwa na muda wa haraka zaidi katika mbio za mita 60 kwa Marekani kwa umri wake, alianza kukimbia ili kukabiliana na vifo vya wanawe wawili wa kiume na ameendelea kwa usaidizi wa binti yake akiwa kama kocha wa riadha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents