Habari

Biden atangaza sheria mpya za chanjo

Rais wa Marekani Joe Biden, ametangaza sheria mpya zinazolenga kuwahamasisha Wamarekani zaidi kupokea chanjo ya Covid-19, huku akionyesha masikitiko juu ya ongezeko la vifo vinavyoweza kuepukika.

Miongoni mwa sheria hizo mpya, wafanyakazi wa Serikali watahitajika kusaini fomu za kuonyesha kuwa wamechomwa chanjo au vinginevyo watii sheria hizo mpya juu ya ulazima wa kuvaa barakoa, upimaji wa kila wiki, kukaa umbali wa angalau mita 2 baina ya mtu na mtu miongoni mwa sheria nyengine.

Rais Biden amesema, “Hili sio suala la majimbo mekundu au ya samawati. Ni suala la kufa au kupona. Ndio hivyo. Najua kuna watu wanaozungumzia juu ya uhuru lakini wakati nikiwa shule pamoja na mafunzo niliyopata kutoka kwa wazazi wangu, uhuru unakuja na jukumu. Uamuzi wako wa kutochanjwa unaathiri mtu mwengine. Watu ambao bado hawajapokea chanjo wanaeneza virusi.

Sheria hizo zinalenga kuongeza idadi ya watu kupokea chanjo ya Covid-19 miongoni mwa wafanyakazi wa serikali, na pia kuwa kama mfano kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.Hata hivyo, sheria hizo huenda zikaibua shutma kali hasa kutokana na mjadala mkali wa kisiasa unaoendelea nchini humo juu ya uwezo wa serikali wa kuwahamasisha Wamarekani kufuatia sheria za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents