Habari

Biden kusaini maagizo 12 ya rais, kuanza na mizozo hii mikubwa minne

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushughulikia janga la virusi vya Corona, Uchumi wa nchi hiyo unaodorora, Mabadiliko ya hali ya hewa na Ubaguzi wa rangi.

Haya ni kwa mujibu wa mkuu wa utumishi anayetarajiwa Ron Klain. Katika taarifa aliyoitoa jana Jumamosi, Klain amesema kuwa mizozo yote hii inahitaji kushughulikiwa kwa haraka na kuongeza kuwa Biden atatia saini takriban maagizo 12 ya rais baada ya kuapishwa siku ya Jumatano.

Klain aliongeza kuwa katika siku zake 10 za kwanza ofisini, Biden atachukua hatua madhubuti kushughulikia mizozo hiyo minne, kuzuia madhara mengine ya haraka na yasiyoweza kurekebishwa, na kurudisha nafasi ya Marekani ulimwenguni.

Joe Biden anatarajiwa kuapishwa Januari 20, 2021 kuwa Rais wa 46 wa taifa la Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents