Burudani

Big Brother Africa: Wanaume wapeana uzoefu wa ‘maisha magumu’ waliyoyaacha nyumbani

Wote tunafahamu kuwa Big Brother ni mchezo, of course ni shindano sababu lina zawadi kwa mshindi atakayepatikana mwishoni (siku ya 91). Lakini kati ya washiriki wote 28 kila mmoja alichukua fomu za kushiriki kwa sababu zake binafsi, wapo ambao huko wanakotoka wanamaisha mazuri na wameenda mjengoni kwaajili ya kuhave fun, na wapo ambao wamechukulia kama fursa ya kuboresha maisha yao endapo watabahatika kushinda.

Mapema wiki hii Hakeem, Bolt, Nando na Bimp wakiwa nje ya nyumba eneo la garden walibadishana uzoefu wa maisha ya kila mmoja wao huko alikotoka, na hapa ndipo jibu la kwanini kila mmoja wao yupo mjengoni iliweza kuonekana.

Bimp
Bimp

Bimp mshiriki wa Ethiopia ni moja kati ya washiriki ambao bila ubishi yuko mjengoni kwasababu anahitaji kushinda kile kitita cha biggie (huenda hata zaidi ya wengine sababu ameamua kuzungumza) sababu amechoshwa na ugumu wa maisha ambao humfanya aombe ombe pesa kwa marafiki zake na familia kwaajili ya kukidhi mahitaji yake ya kila siku. Bimp alikili kuwa ana ndoto inayootwa na kila binadamu (kuwa tajiri) ili aweze kumfanya mama yake awe na maisha mazuri pia. (Nahisi ameshaifanyia bajeti ya ndotoni $300,000).

hakeem
Hakeem

Hakeem wa Zimbabwe yeye hakuwa mbali sana na Bimp sababu aliamua kuwatajia samani chache alizonazo chumbani kwake, na kuongeza kuwa ameanza utafutaji akiwa na umri mdogo na hivi sasa hataki mama yake ateseke kwa sababu yake.

bolt3
Bolt

Bolt ambaye ameonekana kutopendwa na washiriki wengine hivi karibuni hapa alionekana kuwa ndio mwenye neema zaidi! (angalau kwa hao aliokuwa nao). Bolt ni kati ya wale wachache ambao maisha yao ni mazuri huko Sierra Leone. Lakini akiwa na wanaume wenzie hakutumia muda huo kujisifia lakini kutoa ushauri wa jinsi ya kuhustle bila kukata tamaa kama mwanaume. Alisisitiza kuwa kama mtu uki hustle basi lazima njia za mafanikio zitafunguka (nahisi aliongea kwa uzoefu).

Pia alikili kuwa na maisha mazuri na ya kifahari, magari na pesa nyingi huko kwao lakini havikuja hivi hivi ni baada ya kuvuka milima na mabonde hatimaye maisha yakamnyookea.

Hii ni sehemu ya faida chanya za mchezo wa big brother ambao unakutanisha watu tofauti, kutoka nchi tofauti, wenye makuzi tofauti, tabia tofauti na wenye uzoefu tofauti katika maisha, hivyo kila mmoja wao anaweza kujifunza kitu kutoka kwa mwenzie ambacho kinaweza kumsaidia katika maisha yake ya baada ya ‘The Chase’.

Hata mtu asiposhinda ana nafasi kubwa sana ya kupata fursa zingine kutokana na ukweli kwamba kushiriki tu katika reality show hiyo inaweza kumpa mtu connection kubwa na za maana mara baada ya shindano sababu ni njia nzuri ya kuonesha kipaji na kukuza majina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents