Burudani

Bilionea anayempeleka Diamond Ghana, Ndege ya Diamond ina jina lake (Video)

Bilionea anayewapeleka Diamond, Davido na mastaa wengine Ghana kwenye Birthday yake ya kutimiza miaka 40 anaitwa Richard Nii Armah Quaye @richardniiarmahquaye

Huyu ni mjasiriamali na mwekezaji kutoka Ghana, anayejulikana kwa kuanzisha na kuongoza kampuni mbalimbali. Alizaliwa tarehe 21 Machi 1984 katika eneo la Jamestown, Mkoa wa Greater Accra, Ghana.

Mnamo Mei 2019, alianzisha Quick Angels Limited, kampuni inayotoa msaada wa kifedha kwa biashara changa na kuendeleza ujasiriamali nchini Ghana. Kupitia kampuni hii, amewekeza katika biashara kama Pizzaman-Chickenman, Ridge Medical Center, Doughman Foods, na nyinginezo.

Moja ya story ya kusisimua kuhusu Quaye ni kwamba:- Kabla ya mafanikio yake, Quaye alifanya kazi mbalimbali za kujikimu, ikiwemo kuosha vyombo 5,000 kwa siku na kuuza pombe za kienyeji katika eneo la Jamestown baada ya kumaliza shule ya sekondari. Alipofikia umri wa miaka 27, alikuwa amepata dola milioni moja ya kwanza kutokana na juhudi zake za kibiashara.

Kuhusu utajiri wake wa sasa, ingawa thamani yake kamili haijulikani hadharani, taarifa zinaonyesha kuwa hivi karibuni alinunua gari la kifahari aina ya Bugatti Chiron na ndege binafsi aina ya Gulfstream G200 Galaxy, hatua inayoashiria uwezo wake mkubwa wa kifedha.

Hata Ndege anayoipanda Diamond ndio ile ile aliyoinunua yeye na hata jina la Ndege limeandikwa RNAQ40 likimaanisha maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa Richard Nii Armah Quaye.

Huenda amemtumia Diamond Ndege imfuate Tanzania.

Swipe kuiona hiyo ndege ya Gulfstream G200 Galaxy ambapo gharama yake ni kuanzia dola milioni 7 hadi dola milioni 10 ambayo ni sawa na TZS 16.1 bilioni mpaka TZS 23 bilioni.

Imeandikwa na @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents