Michezo

Bilionea mpya wa Newcastle United aanza na wachezaji wanne wa Man United

Baada ya Klabu ya Newcastle United kuchukuliwa na tajiri wa mafuta, mwana wa mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman lengo la kwanza katika dirisha la usajili ujao ni kuwango’a wachezaji wanne wa Manchester United.

Katika kuonesha kuwa hawana muda wa kupoteza, Newcastle inatarajia kuanza na vijana hao wa Ole Gunnar Solskjaer ili nayo ijijengee utawala wake kama ilivyo kwa Manchester City.

Wachezaji hao wanaolengwa wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa ni Jesse Lingard, Donny van de Beek, Anthony Martial na Eric Bailly.

Siku ya Jumamosi ilithibitishwa rasmi kuwa klabu ya Newcastle United imepata mmiliki mwingine. Taarifa rasmi kutoka Premier League zilithibitisha hilo.

Related Articles

Back to top button